Kocha mkuu wa Al Ahly ya Misri, Jess Thorup ameahidi kuibeba Yanga na kufuzu robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika kwani anapambana kupata ushindi dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco katika mchezo wa mwisho ambapo Yanga inatakiwa kushinda dhidi ya JS Kabylie ya Algeria.
“Sijaridhishwa na tulivyocheza leo, (jana).
Ni vile tumetuzu robo ambacho ndio ilikuwa muhimu...! Jumapili tunacheza vs AS FAR na tutatakiwa kuonesha tupo serious na mashindano..
Tunatakiwa kuamua tuongoze kundi na si
vinginevyo..! Tutalazimisha kushinda na itatakiwa iwe hivyo...!
Ni lazima tushinde”, amesema Jess Thorup kocha wa Al Ahly
