Licha ya Simba SC inayoshiriki Ligi Kuu bara kushinda mabao 3-0 na kuendelea na mashindano ya kombe la CRDB, lakini timu nyingine ya Ligi Kuu bara kuondoshwa katika michuano hiyo na timu ya daraja la chini ni KMC baada ya kufungwa mabao 3-2 kwa mikwaju ya penalti.
KMC waliondoshwa na timu ya first League, Bandari Tanzania kufuatia sare ya mabao 3-3 kwenye uwanja wa Filbert Bayi uliopo Kibaha mkoani Pwani.
Matokeo ya michezo ya hatua ya 64 Bora CRDB Bank Federation Cup 2025/2026.
