Aliyekuwa winga wa klabu ya Azam FC na MC Alger raia wa Ivory Coast Kipre Zuon Junior amejiunga na klabu ya Al Nasry ya Ligi Kuu ya Libya,
Kipre Jr amejiunga na klabu ya Al Nasry baada ya kuachana na waliokuwa waajiri wake MC Alger kwa makubaliano ya pande zote mbili,
Sasa rasmi amejiunga na klabu ya Al Nasry kwa mkataba wa msimu mmoja na nusu,
Kipre Jr anaungana na Fabrice Ngoma, Nathan Fasika, Steve Mukwala na Khadim Diam ambao wote wamesajiliwa Al Nasry
