Mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba, Kibu Dennis jana alifanikiwa rasmi kucheza mchezo wake wa kwanza akiwa na klabu yake mpya ya Al Nasry ya Libya.
Kibu Dennis aliingia kwenye dakika ya 71 ndani ya mchezo huo ambao Al Nasry iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Al Murooj kwenye mchezo wa group 4 ligi kuu ya Libya.
Kwa upande mwengine pia wachezaji wengine wa zamani wa Simba, Steven Mukwala pamoja na Fabrice Ngoma nao pia walikuwa sehemu ya mchezo huo.
Fabrice Ngoma alianza kwenye kikosi cha kwanza cha mchezo huo na kucheza dakika zote 90 huku Steven Mukwala akiingia kwenye dakika ya 71 ndani ya mchezo huo.
