Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) linalaani vikali matukio yasiyokubalika yaliyotokea wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa kati ya Al Ahly ya Misri na ASFAR ya Morocco mjini Cairo Jumapili, Februari 15, 2026.
CAF imelipeleka suala hilo kwenye Bodi ya Nidhamu kwa uchunguzi na imetaka hatua stahiki zichukuliwe kwa watakaobainika kuhusika baada ya Mashabiki kutupa chupa ndani ya Uwanja na kuzua vurugu.
Katika mchezo huo timu zote zilitoka sare ya 0-0 na kutinga hatua ya robo fainali ya klabu Bingwa Afrika.
