Ruka hadi kwenye maudhui makuu

JUMA SAID NYOSO: BEKI MTUKUTU UWANJANI ALIYEPITA ASHANTI, SIMBA SC, MBEYA CITY NA KAGERA SUGAR

Na Abdul Makambo
0787905328.

JINA la Juma Said Nyoso si geni kwa wapenda soka hapa nchini pi ni jina maarufu katika masuala haya ya mchezo wa soka.

Nyoso ni beki au mlinzi wa kati akizimudu namba 4 na 5, miaka ya katikati ya miaka ya 2000 aliibukia kwenye Ligi Kuu bara akiwa kwenye klabu ya Ashanti ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Akiwa Ashanti ndipo alipoonekana na kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars miaka ile Mbrazil Marcio Maximo na kumuita kwenye kikosi cha National team.

Juma Nyoso


Nyoso ni beki makini wa kati na ana ball control na mtulivu wakati
mwingine anacheza soka la kistaarabu kutegemea na mechi lakini kama mechi kubwa kubwa anakua ni mtu hatari na asiependa masihara kiwanjani.

Kuna kipindi fulani akiwa Simba alikua pacha wake ni Kelvin Yondan "Vidic"' na hata kwenye timu ya taifa, Taifa Stars pia alikua anasimama na Yondan.

Washambuliaji wengi hapa nchini wamekua wanamhofia Nyoso, hata John Bocco na Meddy Kagere walikua wanapata wakati mgumu wakikutana na Nyoso.

Hata kuna wakati fulani Yanga ikicheza na timu ya Mbeya City mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele alikua anakabwa na kusukumwa halafu alikua hamuangalii usoni zote ni mbinu za kimchezo mshambuliaji akuogope.



Nyoso alikua ni beki mwenye mikwala kiwanjani alikua anafuata nyayo za mabeki wa zamani kama Omary Chogo na Mohamed Kajole wa Simba na Omary Kapera, Athumani Kilambo na Salum Kabunda wa Yanga.

Bila shaka wasomaji wa Mambo Uwanjani Blog mumemfahamu Juma Said Nyoso.beki wa zamani wa kimataifa wa Tanzania ambaye hatosahaulika kwa matukio yake ikiwemo la kunshika makalioni mshambuliaji wa Simba na Azam FC, John Bocco ambalo lilipelekea mpaka kufungiwa na Bodi ya Ligi, TPLB.




Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa