Ruka hadi kwenye maudhui makuu

GSM na MO wote msaada kwa timu zao, ila mmoja ana nidhamu, mwingine mhuni...

Nimewafuatilia GSM na Mo ni matajiri wakubwa Tanzania, wote wana mchango mkubwa sana kwa timu zao

Huwezi kutaja maendeleo ya Yanga bila GSM huwezi kutaja maendeleo ya Simba bila Mo

Kinachoifanya Yanga kutamba sa hivi ni busara za GSM anajua mipaka yake na anaijua kazi yake vizuri sana

Sijawahi kumuona akitoa tamko lolote au kuingilia jambo lolote pale Yanga sababu kuna mtu wake anamuamini ambaye ni Eng Hersi

Njoo kwa Mo sasa suala la kuingilia utendaji wa timu na kutoa matamko yanayo zua taharuki kwake ni kitu cha kawaida

Tajiri Mo kuna muda aliandika tamko la kususa hadharani, kuna muda pia aliandika tamko kusema kuwa kufungwa goli tano na yanga kuna wachezaji wana hujumu timu bila kuwa na ushahidi wowote, tajiri mo kuna muda aliandika hadharani kuwa simba inahitaji kipa mpya na akamsajili na sijui kipa wake aliishia wapi, juzi hapa kaandika kuulizia mabadiliko ya simba wakati anajua kila kitu kuhusu simba.

Shida ya watu wengi wanafikiri mtu kuwa tajiri ndo kujua kila kitu matokeo yake mo anaweza fanya kitu chochote na watu wakachukulia kitu cha kawaida ila ukiangalia kwa undani kuna madhara yake kuliko faida

Nafikiri ni wakati sasa mo ajifunze kwa gsm aache watu wa mpira wafanye kazi yao bila kuwaingilia bila kutoa matamko yanayoweza kuigawa timu ambayo hayana faida yoyote kwa timu

Nafikiri mashabiki uchwara waliokwenda kumshambulia mangungu wangeenda kumshauri mo kuwa ajifunze kwa GSM


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa