Timu ya Dodoma Jiji imeendelea kutakata kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara inayodhaminiwa na benki ya NBC, baada ya usiku huu kuilaza TRA United mabao 3-0.
Kwa matokeo hayo Dodoma Jiji iliyokuwa nyumbani, imeishusha Simba kwenye nafasi ya sita ikifikisha pointi 20 huku Simba ikiangulia nafasi ya saba na pointi 19.
Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na Faraji Kayanda dakika ya 15, Gadiel Michael dakika ya 40 na William Edgar dakika ya 55.
Edgar amekuwa na mwendelezo mzuri wa kufunga mabao tangu alipoanza kufanya hivyo dhidi ya Yanga na kupelekea kupewa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu bara.
