Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara inayodhaminiwa na benki ya NBC, Yanga SC usiku huu imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo FC katika uwanja wa Majaliwa Stadium, Ruangwa mkoani Lindi.
Bao pekee lililowapa pointi 3 Yanga SC limefungwa na mshambuliaji wao hatari raia wa Angola, Laurindo Dilson Maria Aurelio Depu dakika ya 26 kwa changamoto ya penalti.
Kwa matokeo hayo sasa Yanga SC imefikisha alama 25 ilipanda hadi nafasi ya pili nyuma ya JKT Tanzania inayoongoza ikiwa na alama 28, kwa mwenendo wa Yanga inaweza kutetea taji lake msimu huu ikiwa ni kwa mara ya Tano mfululizo.
