Timu ya Azam FC usiku huu imepata ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya Nairobi United ya Kenya mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika uwanja wa New Amaan Stadium, Zanzibar.
Bao pekee lililowapa ushindi Azam FC limefungwa na kiungo mshambuliaji Feisal Salum "Feitoto" dakika ya 11.
Kwa matokeo hayo Azam FC imefikisha pointi 6 ikicheza mechi 4 huku ikiwa imefufua matumaini ya kuingia robo fainali.
