Umekua msimu mbaya kwetu kwenye michuano ya kimataifa, inauma lakin hatuna budi kukubali kuwa msimu huu umekua mgumu kwetu
Kama ambavyo misimu mingine tunafuzu kwenda Robo Fainali na wengine wanashindwa basi msimu imekua zamu yetu kuanguka
Hatuna sababu ya kuvurugana wala kutafuta mchawi itoshe kusema msimu huu haukuwa wetu au haikua rizki yetu
Tumalizie mechi mbili zilizobaki baada ya hapo tuwekeze nguvu kwenye mashindano ya ndani huku bado tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri
Poleni ndugu zangu Wana Simba, Tulichozea kufanya tumeshindwa kufanya safari hii, Tukubali kuwa huu ni msimu mbaya kwetu na hutokea kwa timu yeyote Duniani
Asanteni na poleni wale wote waliotoa nguvu zao kuipambania Simba ishinde hii leo, Asanteni wale wote waliokuja Uwanjani hii leo, Tanatambua na kuthamini mchango wenu kwenye kuipambania Simba yetu
Itoshe kusema Asante Mungu wewe ndio mpangaji wa yote
Hadi wakati mwingine Wanyama, Hakuna kukataa tamaa maisha ya mpira bado yanaendelea
