Nimeona taarifa ya The Guardian ya England kuwa AFCON 2027 inaweza isifanyike sababu ya utayari wa nchi tatu za Afrika Mashariki.
Lakini mara ya mwisho Rais wa CAF Dr Patrice Motsepe aliulizwa kuhusu swali hilo na majibu yake yalikuwa ni kuwa mashindano yatakuwepo na hakuna mpango wa kuondoa mashindano Afrika Mashariki, mkutano wa kesho wa CAF hapa utakuwa kwa ajili ya kuzungumza kuhusu maandalizi ya michuano hiyo.
Dr. Motsepe yuko mstari wa mbele kuhakikisha kila kitu kitakuwa sawa sababu kazi yake ni kukuza mpira wa Afrika.
