Makocha 688 wametuma maombi ya kuifundisha timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ ambayo imekaa mwezi mmoja bila Kocha Mkuu.
Shirikisho la soka la Rwanda (FERWAFA) liliachana na aliyekuwa Kocha wa timu hiyo Adel Amrouche Januari 14, 2026 baada ya kuhudumu kwa mwaka mmoja.
Wakati mchakato wa kutafuta mbadala wake ukiendelea, FERWAFA ilitangaza kupokea maombi ya Makocha 688 wenye sifa, ambayo yatafuatiwa na hatua ya mchujo kwa kuzingatia sifa na uzoefu wa kufundisha timu za taifa na ushiriki wao katika michuano mikubwa ikiwemo Kombe la Mataifa ya Afrika na Kombe la Dunia.
Rwanda itaandaa mechi za kirafiki za FIFA huko Kigali Machi 2026.
Katika michezo hiyo, Rwanda ipo Kundi A pamoja na Estonia, Grenada na Kenya, huku Kundi B likiwa na timu za Aruba, Liechtenstein, Macau na Tanzania.
