Kikosi cha Yanga SC kimeianza safari alfajiri leo kuelekea nchini Misri kuifuata Al Ahly kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).
Mechi hiyo itapigwa Ijumaa Januari 23, 2026 saa 1:00 usiku huku ikisafiri na nyota wake wote waliotangazwa na wale waliokuwa nje ya timu kwa majukumu ya timu za taifa.



