Kiungo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Alphonce Mabula anahusishwa na vilabu vingi ambavyo vinahitaji saini yake kwasasa zikiwemo Simba na Yanga.
Mabula alikiwasha sana akiwa na kikosi cha timu ya taifa, AFCON pale Morocco kiasi ambacho kimepelekea klabu yake ya Shamak kutaka kumuongezea mchezaji huyo mkataba kwa haraka mno.
Ikumbukwe kuwa mchezaji huyo mkataba wake unatamanika mwisho wa msimu huu na klabu yake, bado hajasaini mkataba mpya ila klabu bado ina push kukamilisha dili hilo.
Wakala wa mchezaji bado anaendelea kuchakata ofa zilizopo mezani ili kuona ni sehemu gani itakuwa sahihi kwa mchezaji ingawa vigogo Simba na Yanga nao wameonesha nia ya kumsajili
