Timu ya Yanga Princess haitaki utani kabisa na Ligi Kuu ya wanawake Tanzania bara, baada ya kuilaza Bilo Queens mabao 2-0 mchezo wa ugenini huku ikiendelea kuisogelea Simba Queens inayoongoza ligi.
Mabao ya Yanga Princess yamefungwa na Aregash dakika ya 02 na mshambuliaji wa zamani wa Simba Queens, Aisha Djafar dakika ya 25, Yanga Princess imefikisha pointi 27 ikiwa nyuma ya Simba Queens.

