Rais wa Shirikisho la soka la Ujerumani (DFB), amesema ni wakati wakati wa kujiondoa kwenye Kombe la Dunia la 2026 kutokana na hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump.
Marekani itakuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia msimu wa joto mwaka huu, pamoja na Canada na Mexico.
Mapema mwezi huu, Rais Trump aliwakasirisha viongozi wa Ulaya kwenye mkutano kuhusu azma yake ya kutwaa Greenland, ambayo sasa inasimamiwa na Denmark.
Kati ya mechi 104 katika kombe la Dunia la 2026, 78 zitafanyika nchini Marekani.
Itakumbukwa kuwa Marekani iliwahi kuzihimiza nchi nyingine kususia michezo ya Olimpiki ya 1980 kwa sababu Muungano wa Kisovieti kuivamia Afghanistan.
