Timu ya Simba Queens imeendelea kuunyemelea ubingwa wa Ligi Kuu ya wanawake Tanzania bara baada ya jioni ya leo kuilaza Geita Queens mabao 4-0 uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
Kwa matokeo hayo Simba Queens imefikisha pointi 31 ikicheza mechi 11 huku watani zao Yanga Princess wakiwa na alama 27 mechi 10.
Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Jenitrix Shikangwa aliyefunga hat trick ya mabao matatu na moja lilifungwa na Zawadi Usanese.


