Timu ya Simba Queens imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu bara ya wanawake baada ya kuilaza Alliance Girls bao 1-0 mechi ikichezwa ugenini.
Kwa matokeo hayo Simba Queens inaendelea kutanua kileleni ikifikisha pointi 28 na mechi 10 wakati anayefuata Yanga Princess ikiwa na pointi 24 na mechi 9.
