Kocha Mkuu wa klabu ya Transit Camp kutoka jijini Dar es salaam, Shadrack Nsajigwa raia wa Tanzania, ameibuka kuwa kocha bora wa mwezi Disemba mwaka jana katika ligi ya NBC Championship.
Kocha huyo aliiongoza timu hiyo kwenye michezo mitano bila kupoteza mchezo wowote huku akiweka rekodi ya kushinda michezo mingi mfululizo kwa Championship msimu huu.
Kutokana na ubora wake timu hiyo ilipaa mpaka nafasi ya tatu licha sasa imeshuka mpaka nafasi ya nne baada ya kupoteza katika mchezo wa mwanzoni mwa mwaka huu.
Nsajigwa amewashinda kocha mkuu wa Geita Gold kutoka mkoani Geita Zuberi Katwila na kocha wa Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera Juma Kaseja ambaye aliingianao katika hatua ya Fainali.
Kocha Nsajigwa ameibadilisha sana Transit Camp msimu huu ikiwa na matokeo bora sana kiwanjani na mpaka sasa ipo nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi ya NBC Championship ikiwa na alama 33.
