Mshambuliaji wa timu ya Tanzania Prison na timu ya taifa ya soka la ufukweni Samuel Mbangula ametoa shukrani za dhati kwa madaktari na wataalamu wa tiba baada ya kufanikiwa kupona majeraha yaliyomweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Mbangula alionekana kuwa na furaha kubwa kurejea kikosini, na katika ujumbe wake kupitia fulana aliyoivaa ndani ya jezi wakati wa mmoja kati ya mechi, aliandika "Asante Dr. Abbas, Asante Dr. Lanina, Ee Mwenyezi Mungu, nashukuru kwa kila jambo".
Alishukuru kwa utaalamu na uangalizi wa karibu aliopata kutoka kwa madaktari hao wawili, akionyesha kuwa walikuwa nguzo muhimu katika kipindi chake cha kurejea kwenye hali ya kawaida (rehabilitation).
Kipindi cha majeraha huwa ni kigumu kwa wachezaji kiakili, lakini msaada wa kitabibu humsaidia mchezaji kubaki na matumaini.
