TIMU ya Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Bahati mbaya kwao Pamba Jiji waliokaribia kupata sare ya ugenini walijifunga wenyewe dakika ya 90'+3 kupitia kwa mshambuliaji wao, James Mwashinga.
Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar wanafikisha pointi 17 katika mchezo wa 11 na kusogea nafasi ya tatu kutoka ya tano, wakati Pamba Jiji FC inabaki na pointi zake 16 za mechi 10 sasa ikishuka kwa nafasi moja hadi ya nne.
