Klabu ya AIK inayoshiriki Ligi kuu nchini Sweden imemtambulisha Kiungo Mshambuliaji Kinda wa Kitanzania Anaemudu kucheza kama Mshambuliaji pia Mohamed Shilla Kwa mkataba maalumu wa miaka Minne hadi 2030 ambapo ataanzia Kutumikia Timu za vijana huku akiangaliwa uwezekano wa kupandishwa Timu kubwa
Mohamed ni miongoni mwa vijana waliotoka Azam na kwenda kufanya majaribio klabuni hapo ikiwa ni matunda ya Mahusiano baina ya Vilabu hivyo Viwili
