Mshambuliaji (Forward) Thomas Ulimwengu amekamilisha kusaini mkataba wa nusu msimu wa kuitumikia klabu ya Coastal Union ya Tanga.
Ulimwengu anatarajiwa kutambulishwa rasmi muda wowote kuanzia sasa, hatua inayoongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Coastal Union kuelekea hatua ya pili ya msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akiwa na uzoefu wa juu wa mashindano ya kimataifa, Ulimwengu ni mshindi wa Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na CAF Super Cup akiwa na TP Mazembe mafanikio yanayoakisi kiwango na uthabiti wa mchezaji katika soka la Afrika.
