Mara baada ya klabu ya Simba Sc kufanikiwa kuinasa saini ya aliyekua kiungo mshambuliaji wa klabu ya Singida Black Stars Clatous Chota Chama, mashabiki wa klabu ya Simba Sc wameonyesha wazi matamanio yao ya kutaka kuona viongozi wao wanafanya jitihada za kuinasa saini ya kiungo mkabaji wa klabu hiyo raia wa Uganda anayejulikana kwa majina ya Khalid Aucho.
Khalid Aucho ni moja kati ya mastaa wa klabu ya Singida Black Stars ambao wamempongeza Chama kujiunga na klabu ya Simba Sc na salamu zake za pongezi amezichapisha kwenye ukurasa rasmi wa Instagram unaotumiwa na Clatous Chota Chama.
Mara baada ya Aucho kumpongeza Chama kwa kusajiliwa na klabu ya Simba Sc, mashabiki wa klabu ya Simba Sc wametimia nafasi hiyo kumuomba Aucho aungane na Chama kwenye kikosi chao ambacho kinaonyesha kuwa na madhaifu mengi msimu huu haswa kwenye eneo la kiungo.
Mashabiki hao wameonyesha kuvutiwa zaidi na ubora wa Khalid Aucho na wanaamini kwamba huyu ni mchezaji wa daraja la juu sana ambaye kama atasajiliwa na viongozi wa klabu yao basi anaweza kuongeza kitu kikubwa sana kwenye eneo lao la kiungo.
Khalid Aucho hajataka kupepesa macho kwenye sakata hili bali ameibuka na kujibu maombi ya mashabiki wa klabu ya Simba Sc kwa kuweka emoji za kucheka akiwa na maana kwamba amefurahishwa na kile ambacho mashabiki hao wamekifanya.
Khalid Aucho mpaka sasa bado ni mchezaji halali wa klabu ya Singida Black Stars lakini Simba Sc bado wanayo nafasi ya kupambana zaidi kama watakuwa wanahitaji saini yake haswa katika dirisha hili la usajili kwani nyota huyo hana changamoto ya kuchagua timu ya kuitumikia bali anaangalia maslahi.

