Na Abdul Makambo
MAKUMBI Juma Baruani ni mmoja wa washambuliaji hatari kuwahi kutokea hapa nchini, sifa ya Makumbi ilikua ni ufungaji wa magoli na uwanjani alikua anamudu kucheza namba 9 na alikua ni hatari kwa mabeki wa timu pinzani.
Makumbi ni mzaliwa wa Uvinza mkoani Kigoma na jina lake lilianza kusikika katika medani ya soka tokea miaka ya 1980 akiichezea Pamba Jiji ya Mwanza na 1982 akachukuliwa na klabu ya Yanga SC ya jijini Dar es Salaam.
Makumbi alikua ni hatari ukimtangulizia tu mpira utaona nyavu zinatingishika.
Mabeki wengi hapa nchini na Afrika mashariki walikua wanamhofia kwa uwezo wake aliokuanao wa kufunga magoli.
Mabeki wa hapa nchini akina Shaban Mussa, Lila Shomari, Jellah Mtagwa, Mohamed Rishard, Rashid Idd, Peter Mhina, Mhando Mdeve, Joram Mwakatika na wa nje akina John Bob Ogolla, Josephat Murila.
Tareq Ahmed Adam, Mike Weche na wengineo.leo tunawakosa kuwa na washambuliaji hatari kama Makumbi Juma alijaaliwa kuwa na jicho la kuliangalia goli.
Makumbi alikua ni hatari tokea miaka ya 1982~1983~1984~1985~1990~1991.Pia alikua ni tegemeo la timu ya Taifa~Taifa Stars.
Makumbi ni mdogo wake nyota wa zamani wa klabu ya Simba Sports Club Abuu Juma.
Bila shaka wasomaji wetu wa mtandao wa Mambo Uwanjani Blog watakua wamemfahamu kwa kina mshambuliaji huyu wa zamani wa klabu Young Africans, alikua ni hatari ukimsahau tu utamkuta anashangilia goli kutokana na pasi alizokua anapikiwa na Charles Boniface Mkwasa, Juma Mkambi na Omary Hussein "Keegan".
Huyo ndio Makumbi Juma mshambuliaji hatari wa zamani wa kimataifa wa Tanzania
Ahsanteni
