Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kocha wa Taifa Stars atimuliwa Rwanda


Shirikisho la soka nchini Rwanda FERWAFA, limetangaza kumfuta kazi Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Rwanda, AMAVUBI Adel Amrouche kwa matokeo mabaya.

Adel alishinda mchezo mmoja kati ya minane akiwa Kocha, FERWAFA inasema hakuheshimu baadhi ya masharti ya mkataba wake na alipewa muda wa kuyarekebisha lakini ikashindikana.

Amrouche, aliteuliwa kuwa Kocha wa Amavubi mnamo Machi 2025 kwa kandarasi ya miaka miwili.

Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa uamuzi huo wa haraka unafuatia kuzorota kwa mahusiano kati ya Kocha huyo na baadhi ya Viongozi wakuu ndani ya Shirikisho hilo.