Timu ya Esperance de Tunis ya Tunisia usiku huu imezidi kulizamisha jahazi la Simba baada ya kuifunga bao 1-0 mchezo wa makundi Ligi ya mabingwa Afrika.
Bao pekee la Esperance de Tunis limefungwa na Jack Diarra raia wa Burkina Faso anakotoka mchezaji wa zamani wa Yanga, Aziz Ki, dakika ya 21 kipindi cha kwanza ambalo limedumu mpaka mwisho wa mchezo.
Simba leo imeweka rekodi ya aina yake katika siku za karibuni timu hiyo kupoteza mechi 3 mfululizo kwani hadi sasa haina pointi hata moja.
