KIPA Djigui Diarra amejiunga na timu yake, Yanga leo baada ya mapumziko mafupi kufuatia Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 ambako aliisaidia timu yake, Mali kufika Robo Fainali na kutolewa na Senegal walioibuka mabingwa kwa kuchapwa 1-0.
Kikosi cha Yanga SC kinatarajiwa kuondoka nchini Alfajir ya keshokutwa kwenda Misri kwa ajili ya mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Al Ahly Ijumaa kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo.




