Klabu ya Simba SC imefanikiwa kumrejesha kiungo mshambuliaji wake wa zamani Clatous Chota Chama "Triple C" au Mwamba wa Lusaka kwa kandarasi ya mwaka mmoja akitokea klabu ya Singida Black Stars.
Taarifa zenye uhakika, mchezaji huyo atatambulishwa na Simba muda wowote kuanzia sasa, na huenda Simba ikarejea kwenye makali yake kwani Chama ni bora zaidi katika kutengeneza nafasi za kufunga.
Ikumbukwe kabla ya kurejea Simba, Chama alikuwa anaichezea Yanga aliyodumu nayo msimu mmoja kama ajajiunga na Singida Black Stars.
