TIMU ya Azam FC imelazimishwa sare ya bila mabao na Fountain Gate FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Azam
Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ifikishe pointi 13 katika mchezo wa saba na kusogea nafasi ya tano kutoka ya sita, wakati Fountain Gate inatimiza pointi 11 katika mchezo wa 11, ingawa inabaki nafasi ya tisa kwenye Ligi ya timu 16.
Baada ya mechi hiyo, Azam FC inatarajiwa kusafiri kwenda Kenya kwa ajili ya mchezo wa Kundi B Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Nairobi United Jumapili kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa wa Nyayo Jijini Nairobi.
