Kipindi cha kwanza Yanga waliingia na mfumo wa 3-4-2-1 kisha dakika ya 56 waka-switch kwenda kwenye 4-3-3 baada ya ingizo la Pacome na Muda.
Kipindi cha kwanza kwenye mfumo wa 3-4-2-1 Yanga walizuia vizuri sana na idadi ya wachezaji 7 (Job,Nondo,Bacca,Boka na Mwenda kisha mbele yao kulikuwa na viungo wawili wazuiaji Duke na Damaro)
mfumo huo pia uliwapa balance ya kushambulia na idadi kubwa ya watu 5 (Boka,Mwenda,Okello,Maxi na Depu) na kama Yanga wangekuwa makini mbele ya lango kipindi cha kwanza wangepata goli 2 ile nafasi ya Okello na Maxi zilitakiwa kuingia ndani.
Nadhani ukiachana na kukosa nafasi za wazi Yanga bado wali-switch off kwenye baadhi ya nyakati kitu ambacho kimewafanya Al Ahly kupata nafasi na kutoa kichapo.
Kipindi cha pili Ahly waliongeza kasi na ubunifu huku wakipeleka mipira mingi kwa nahodha wao Mohamed Trezeguet ambae alikuwa na hatari sana kwenye defense ya Yanga.
Damaro,Muda na Mwwnda hawakuwa na mechi bora
Marwan Osman,Trezeguet na Emam Ashour wanajua sana Ball
Nondo alitulia sana jana
Depu anaenjoy sana kucheza kama target man….jamaa ana nguvu sana kwenye mapambano
Yanga wamepoteza mechi ila kuna progress kubwa sana kwenye timu yao
