Wakala wa Kocha wa Yanga, Romain Folz, amefichua kuwa ili klabu hiyo iweze kuvunja mkataba na kocha huyo, italazimika kulipa fidia ya takribani Dola za Kimarekani 150,000 (sawa na Shilingi milioni 380 za Kitanzania).
Kwa mujibu wa wakala huyo, Folz bado ana mkataba halali na Yanga, hivyo hatua yoyote ya kuvunja makubaliano hayo kabla ya muda wake kumalizika italazimu klabu hiyo kulipa kiasi hicho cha fidia.
Taarifa hiyo imezidi kuchochea mvutajo baina ya pande hizo mbili upande wa mabosi wa Yanga wanaoomba kocha huyo avunje mwenyewe mkataba, hasa ikizingatiwa kuwa kumekuwa kushuka kwa maelewano katika benchi la ufundi la Yanga kufuatia kiwango kibovu cha hivi karibuni.