Baadhi ya viongozi wa Yanga ndani ya Kamati ya Utendaji wamependekeza mechi ya marudiano na Sliver Strikers ichezwe Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Wameweka mezani hoja.Jambo linachakatwa kupata maamuzi ya pamoja.
Mara ya mwisho Yanga kutumia Uwanja wa New Aman Complex mechi za CAF waliibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhii ya CBE. Ikiwa ni hatua kama hii ya mechi ya mwisho kwenda makundi.
Kumbukumbu mbaya kwa Yanga ni kushindwa kupata walau goli moja dhidi ya MC Alger kupelekea kutupwa nje, hatua ya makundi mbungi ikipigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.