Kaimu kocha mkuu wa Yanga SC, Patrick Mabedi amesema katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Silver Strickers, watashambulia mwanzo mwisho-.
"Kesho tunatakiwa kushambulia tu hatutakiwi kukaa nyuma. Tayari wapinzani wetu wako mbele kwa goli moja na tunatakiwa kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho ili tusonge mbele na huo ndo ukweli na wala hakuna njia nyingine",
"Kwenye mpira kila mchezo una presha na sisi tunaishi kwenye hiyo presha na tunajua kuna presha kubwa hasa kwa mashabiki wetu lakini jambo la muhimu kwenye mchezo wa kesho nikufanya vizuri na kusonga mbele ili kuondoa hiyo presha na Wachezaji wote wamejiandaa vizuri na wako tayari kuipambannia nembo ya Klabu yetu”
Tulianza kambi yetu Jumanne baada ya mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Silver Strikers, Malawi. Wachezaji wamejiandaa vizuri na kuna nguvu kubwa, hamasa na ari baina yao kuelekea mchezo huu muhimu wa kesho",
Amesema Kaimu kocha mkuu wa Yanga SC, Patrick Mabedi