Timu ya Ettiene Ndayiragije ya Polisi FC ya nchini Kenya imefungua malalamiko kwenye Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) wakidai kuwa Al Hilal kwenye mchezo wa pili uliochezwa Benghazi nchini Libya na kupasuka mabao matatu kwa moja walichezesha wachezaji watatu ambao hawakusajiliwa na Shirikisho la Soka nchini Sudan (SFA)
Polisi Kenya walitolewa kwa jumla ya mabao manne kwa moja baada ya kufungwa bao moja wakiwa nyumbani kabla ya kuchakazwa chuma tatu kule nchini Libya.
