Kwa mara nyingine tena uongozi wa klabu ya Singida Black Stars chini ya Mwenyekiti wake Ibrahim Mirambo wanasafirisha Waandishi wa habari na wadau wengine kwenda nje ya nchi kuipa sapoti timu yao.
Gharama zote za Usafiri wa kwenda na kurudi Burundi zipo chini ya Singida Black Stars. Singlda walisafiri na waandishi na wadau kwenda Rwanda wakigharamia kila kitu cha safari, na safari hii kwenda Burundi ambapo watacheza mchezo wa raundi ya 2 ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Flambeau du Centre.