“Tulikuwa tunapiga kelele kwamba Simba yetu hatuelewi inavyocheza lakini sasa imerejea, Simba ya kutisha imerejea, Simba ya kushambulia muda wote imerejea sasa unabaki nyumbani kufanya nini. Na haya sio maneno ya kutoka usingizi, haya ni maneno ya kuona inacheza na pale mwalimu anasema uwanja ulikuwa mdogo. Sasa uwanja wa Mkapa anakwenda kwenye uwanja mkubwa, njoo Uwanja wa Mkapa uonge Simba ikifanya balaa zito.”
“Tuna kila sababu ya kuonyesha utofauti wa sisi na wengine, sisi ndio timu pekee ya Tanzania ambayo imepata ushindi ugenini, Zanzibar sio nje ya Tanzania. Tunayo sababu ya kutamba maana sio rahisi kumtandika bingwa wa Eswatini mabao 3-0. Kila Mwanasimba anawajibu wa kulipa kiingilio chake yeye mwenyewe, naona wengine wameanza kampeni watu waende bure, sasa pamoja na kwamba tumeshashinda mabao matatu twendeni tukaonyeshe nguvu yetu.”
“Mechi ya Oktoba 26 itakuwa mechi ya kumuona Dimitar Pantev halisi akiwa na ukatili kwenye uwanja wa vita. Kwenye mchezo ule wa kwanza mwalimu aliweka wazi kwamba bado hajaridhika na kiwango cha timu yake, kipo kitu mwalimu anakitaka na sisi bado hatujakijua. Sababu mwalimu anasema kwamba hajaridhika na sisi tunakwenda na kaulimbiu ya HATUJARIDHIKA, TUNATAKA ZAIDI.”
“Msiba pekee ndio hauna kiingilio, sisi tunakwenda kwenye starehe lazima kuwe na kiingilio. Huwezi kwenda kumuona mchezaji wa Kombe la Dunia la Vilabu, Seleman Mwalimu, Rushine, Kagoma, Morice, Nangu haiwezi kuwa bure. Siku hiyo sisi tunakwenda kuenjoy, kama una babe wako njoo nae, kama una familia njoo nayo. Hii ni starehe haiwezi kuwa bure.”- Semaji Ahmed Ally.