Nyota wa zamani wa timu ya Sliver Strikers ya nchini Malawi ambaye kwa sasa ni mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa timu ya Silver Strikers Ndugu Peter Pindan amesema ikiwa wamepata ushindi kwenye uwanja wao wa nyumbani, inawezekana pia kupata matokeo kwenye mchezo wa ugenini na kuwatoa Young Africans kwenye mashindano
"Jina langu ni Peter Pindan ni mchezaji wa zamani wa Silver Strikers kwa sasa ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa timu.Ni kweli tumeshinda dhidi ya Young Africans kwenye mashindano ya Caf Champions League.Tutaenda ugenini Tanzania wikiend ijayo, na huenda tukaenda kwenye hatua ya makundi kwani sisi ni moja ya timu bora nchini"
Sisi ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Malawi na pia tunashiriki mashindano ya Caf ina maana sisi ni timu kubwa hakuna timu ndogo inashiriki haya mashindano,
Vijana wako tayari kutetea huu ushindi na chochote kinaweza kutokea kwenye mchezo wa mpira. Tunaenda Tanzania tukiongoza moja bila kwenye mchezo wa kwanza.Nafikiri vijana wapo kwenye haya mashindano kushindana hivyo tunaweza kuwafunga tena"
Peter Pindan amesema hayo katika Mahojiano na Waandishi wa habari