Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imethibitisha kuachana na kocha Nasreddine Nabi kwa makubaliano ya pande zote mbili hivyo kwa sasa kocha huyo wa zamani wa Young Africans Sc yupo huru kujiunga na timu yoyote..
Tayari kocha huyo raia wa Tunisia ameushukuru uongozi wa klabu ya Kaiser Chiefs, wafanyakazi, wachezaji na mashabiki kwa mchango na sapoti yao kwa wakati wote alipokuwa klabuni hapo.