Aliyekuwa kocha wa zamani wa mabingwa wa soka nchini, Yanga SC, Juma Mwambusi amewapasua vichwa viongozj wa klabu hiyo wakiongozwa na Injinia Hersi Said, kwamba Yanga haiitaji kocha wa majaribio isipokuwa inahitaji kocha wa kuendeleza ilipoishia.
"Ukiiangalia Yanga ilivyo sasa haihitaji Kocha wa kujiendeleza au wa majaribio.Inabidi watafute Kocha anaye endana na Yanga ya sasa.Yanga imeshachukua mataji ya Ligi Kuu mara nyingi tu na kwa wachezaji waliopo sasa.
Hata mimi nikipewa ninauchukua ubingwa wa nyumbani bila shida yeyote ile.Ila kama wana malengo ya kufanya kimataifa Viongozi wanapaswa kutafuta Kocha anaye endana na mahitaji ya mashindano husika sio kwa wa majaribio"Juma Mwambusi Kocha wa zamani wa Yanga!