Mkojani kuna kipindi alikuwa yeye ndo comedy yenyewe hapa nchini, Yaani kila sehemu alitamba yeye, kwenye nyumba za watu, mitandaoni, kule you tube ndo usiseme alikuwa akipata views wa kutosha sana.
Yaani ukija kwenye mabasi ya mikoani ndo ilikuwa balaa, kutoka Dar mpaka Mwanza ni muvi za Mkolani tu na watu walikuwa wakifurahia na kuona ni king majuto mpya aliye zaliwa.
Ila kwa sasa kitu cha kushangaza jamaa kapotea ghafla hasikiki tena kila sehemu, najiuliza alipatwa na Nini huyu jamaa?