Kocha wa timu ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini, Mandela Qhogi amesema kwamba katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Simba na kufungwa mabao 3-0, walicheza vizuri zaidi ya Simba ila walichezewa rafu nyingi.
"Tulicheza vizuri kuliko Simba SC, wao muda mwingi walicheza mchezo mchafu kujidondosha kuua moments zetu za kushambulia"
"Naamini ni mbinu wataitumia mchezo wa marudiano kupaki basi na kujidondosha ila tutashambulia kupindua matokeo"
-Mandla Qhogi, kocha mkuu wa klabu ya Nsingizini Hotsupers FC