Kocha mpya wa mabingwa wa soka Tanzania bara Mreno Pedro Goncalves ameanza kazi yake ya kuwanoa mastaa wa timu hiyo inayojiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu bara dhidi ya Mtibwa Sugar.
Pedro Goncalves amechukua mikoba ya Ramon Folz aliyefulushwa hivi karibuni wakati timu ikishiriki Ligi ya mabingwa Afrika raundi ya kwanza ambapo katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Silver Strickers ilifungwa bao 1-0 mjini Lilongwe.


