Na Mwandishi Wetu
KWA Sasa ni marehemu, lakini enzi za uhai wake alijulikana sana kwenye vipindi vya salamu katika vituo kadhaa vya Afrika mashariki, kwa maana nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi ikiwemo Tanzania yenyewe.
Jina lake la kuzaliwa anaitwa Joseph, ila alijulikana kwa jina la Jenerali Mwitakiaro au baba Cevini enzi za uhai wake niliwahi kumuuliza kwanini unajiita Jenerali Mwitakiaro, akajibu Mwitakiaro alikuwa Jenerali wa jeshi la ulinzi wa Tanzania, JWTZ.
Jenerali Ernest Mwita Kiaro alipata kuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi wa Tanzania na alifariki mwaka 1994, Joseph ambaye ni mzaliwa wa Mtwata, Kusini mwa Tanzania ni tofauti kubwa na Mwita Kiaro ambaye ni mzaliwa wa mkoani Mara, kanda ya ziwa, magharibi mwa Tanzania.
Joseph alitokea kuvutiwa na Jenerali Ernest Mwita Kiaro na akaamua kulibadili jina lak e na kujiita Mwitakiaro Joseph alikuwa kinyozi wa nywele katika mitindo mbalimbali ambayo aliiweza.
Mpaka anakutwa na mauti, alikuwa katika saluni moja iliyopo Tabata shule jirani na zahanati ya Tabata shule, kwakweli alikuwa kinyozi mzuri ambaye aliaminika na wengi kuanzia wateja zake na mabosi wa saluni.
Siku ya msiba wake, watu mbalimbali wa maeneo ya Tabata na jirani walikusanyika kumzika fundi huyo mwaminifu, ikumbukwe kwamba katika mafundi wote, kinyozi ndio mwaminifu, kwakuwa unamlipa pesa na anakupa umachokitaka kwa wakati husika.
Jenerali Mwitakiaro alianza kujiingiza kwenye salamu kuanzia mwaka 1999 na aliendelea kudumu kwenye salamu mpaka mwaka 2025 alipofariki.
Kwa maana Jenerali Mwitakiaro alijipatia umaarudu mkubwa kwenye redio za FM na AM kwa maana TBC Taifa, Radio One, Magic FM, Redio Free Africa, EAST Africa, Clouds FM, Wasafi FM, EFM, Uhuru FM, Abood FM na nyinginezo.
Marehemu Mwitakiaro ambaye amefariki akiacha watoto wawili wote wa kike ambapo mtoto mkubwa anasoma darasa la sita na mdogo wake anasoma darasa la pili, alizaliwa miaka ya 1979 na alianza salamu kwenye camp ya Pentagon yenye maskani wake Tabata Mawenzj jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mwanasalamu mwingine aliyefanya salamu kwa ushirikiano mkubwa Nassoro Yusuph amesema Mwitakiaro alianza na Pentagon salamu Club ambapo kipindi hicho walikuwa wanatumia post card.
Yusuph anasema kipindi hicho salamu kwa njia ya post card ilikuwa Radio One, TBC Taifa ambapo wakati huo ikiitwa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Uhuru FM na baadaye Magic FM, lakini mtindo wa post card ulikufa na wakahamia kwenye kupiga simu.
Kwenye club ya Pentagon, marehemu Mwitakiaro alikutana na Yusuph Nindi "Nindiboy", Chief Masanja, Mgosi wa Ndima Muya na wengineo ambao walipata umaarufu kupitia redio.
Lakini pia Jenerali Mwitakiaro alikutana na wanasalamu wengine wa miaka ya 2000 kama akina Nassoro Yusuph, Shukuru Ki Nyange, Omary K Nyange, Shabani Kipresha, Omary Rajabu, Masha Mfinanga, Athuman Mkele, Prince Hoza, Peter Toshiboy, Rajabu Magomba, Grace Michael, Hawa Hassan na wengineo ambao alifanya nao zalamu utadhani wanalipwa.
Jenerali Mwitakiaro amewahi kusafiri mikoa kadhaa hapa nchini na nchi jirani na salamu ndio iliyompeleka, mwanasalamu huyo aligharamiwa kwenda maeneo hayo kutokana na umaarufu wake kupitia redio, kifo chake kimesikitisha wengi ingawa mwenyezi Mungu alimpenda zaidi.
ALAMSIKI