TIMU y JKT Queens imefanikiwa kwenda Fainalimya Ngao ya Jamii Wanawake baada ya ushindi wa penalti 6-5 baada ya sare ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Kiungo mshambuliaji Winfrida Hubert Gerard alianza kuifungia JKT Queens dakika ya 27, kabla ya mshambuliaji Mnyarwanda, Jeannine Mukandayisenga kuisawazishia Yanga Princess dakika ya 44.
Kwenye mikwaju ya penalti waliofunga za JKT Queens ni Esther Mabanza Mpingi, Aaliyah Fikiri Salum, Christer John Bahera,
Deonisya Daniel Minja, Esther Maseke Marwa na Janeth Christopher Pangamwene, wakati Windrida Hubert Gerard alipiga juu ya lango.
Waliofunga penalti za Yanga ni
Jeannine Mukandayisenga, Akudo Esther Ogbona, Aregash Kalsa Tadesse, Precious Christopher Onyinyechi na Uzoamaka Confidence Igwe, huku Angela Michael Chinemere akigongesha nguzo na Agness Sawe Pallangyo akipaisha.
JKT Queens sasa itakutana na Simba Queens katika Fainali Jumapili jioni, wakati Yanga Princess itacheza na Mashujaa Queens kuwania nafasi ya tatu.