Bondia mrembo Debora Mwenda amepata nafasi nyingine ya kupigana Disemba kwa promoter Seleman Semunyu wa kampuni ya Peak Time Media.
Akizungumza na mtandao huu, bondia mrembo amesema, "Nimepata nafasi ya kuwaonesha kua niliamua kuufanya mchezo wa ngumi kwa sababu nina imani ninao uwezo wa kuufanya vizuri mchezo huo, ukiachilia mitazamo mbalimbali ya watu. Tarajieni mazuri kutoka kwangu.
Leo nitawambia maana ya bondia mrembo, urembo unapimwa kwa ujasiri, nidhamu na nguvu ninazo ziweka kila ninapo panda ulingoni na kila ninavyoishi ishi maisha yangu ya kila siku,maandalizi nk. Urembo wangu ni katika moyo wa kupambana na kutokata tamaa.
Kila jasho ni hatua moja karibu na ndoto yangu. Nafanya boxing kwa moyo. Dunia itanikumbuka kama bondia bora wa kike, aliyeinua mchezo kwa nidhamu na mapenzi.