Kiungo wa zamani wa Yanga,Zawadi Mauya,ameshinda kesi yake ya madai dhidi ya Singida,na Sasa klabu hiyo imepewa wiki mbili kumlipa mchezaji huyo pesa zote anazodai.
Mauya aliwashitaki Singida pale (TFF) kwa kushindwa kumlipa mshahara wake wa miezi minne na pesa binafsi ya usajili (sign-on fee) na sasa kesi hiyo imesikilizwa na Mauya ameshinda.
Sasa Singida watatakiwa mumlipa Mauya jumla ya Tsh 66m ndani ya wiki mbili tu.