RAIS wa Yanga SC, Hersi Ally Said amefika makao makuu ya klabu kongwe nchini Brazil, Botafogo yenye maskani yake Ribeirão Preto, Jijini São Paulo.
Akiwa makao makuu ya klabu hiyo ambayo ndio bingwa Brazil kwa sasa — Hersi aliopokewa na Mkurugenzi wa Akademi, Diego Mello ambaye pia Mkurugenzi wa Mahusiano wa klabu hiyo.
Hersi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu Afrika (ACA), pamoja na kujifunza mambo mbalimbali lakini pia aliwaelezea kuhusu Yanga na kubadilishana nao jezi kwa lengo la kujenga mahusiano.