KIKOSI cha Yanga kimeondoka Alfajiri Dar es Salaam Alfajiri ya leo kwenda Angola kwa ajili ya mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji,
Wiliete keshokutwa.
Katika Safari yao, Yanga watapitia Addis Ababa, Ethiopia ambako wataunganisha ndege nyingine hadi
Luanda tayari kwa mchezo wa Ijumaa Uwanja wa Novemba 11, Luanda.
Timu hizo zitarudiana Jumamosi ya Septemba 27 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Elgeco Plus ya Madagascar na Silver Strikers ya Malawi.
Yanga imeondoka saa chache tu baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya watani zao, Simba SC jana jioni katika mchezo wa Ngao ya Jamii Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.